JULIO AWAPIGIA CHAPUO MATOLA, MGUNDA

Na Mwandishi Wetu

"Mimi siogopi kusema ukweli maana naona Azam ina kila kitu, lakini haifanyi vizuri kwa kuwa watu wanaopewa majukumu kuivusha hawawezi, wawape timu watu sahihi ambao wanaujua utendaji lakini wao wanapeana kazi kishkaji sana na ndicho kinachowafelisha"

"Kwa miundombinu iliyonayo Azam hata ikinolewa naye, Juma Mgunda au Seleman Matola wanaweza kuifikisha mbali ikiwemo kutwaa taji la Ligi Kuu kwa mara nyingine kwani ina kila kinachohitajika"

"Wachezaji wanaosajiliwa ni kama hawajitambui na wamekuwa wakiridhikia na pesa nyingi wanazolipwa kwa vile hawana presha wanayopewa kuwafanya wapambane"

"Kwa wanavyocheza uwanjani ukiitazama na Yanga iliyoweka kambi Avic Town Dar es Salaam na Azam iliyotumia pesa nyingi kwenda Tunisia utaona vitu viwili tofauti"

"Yaani Yanga utasema wao ndio walikuwa nje ya nchi kutokana na ubora wa soka wanalocheza kumbe hapana, ila hawa waliosafiri kambi ya wiki mbili, lakini wanapoteza muda mwingi njiani kwenye safari ni lazima wabdilike"

"Namtafuta Idrissa Nassoro (mwenyekiti wa bodi ya klabu) na mtendaji (Abdulkarim Amin ‘Popat’) niwaambie kitu,"

Jamhuri Kihwelu "Julio" (Kushoto)

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA