WENYE LIGI YAO WAREJEA KILELENI NA MWENDO WA 5, 5

Na Asher Maliyaga

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara usiku wa leo imerejea kileleni baada ya kuikandamiza mabao 5-0 timu ya JKT Tanzania katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

Kwa matokeo hayo Yanga inaishusha kileleni Azam FC ambayo jana iliishusha kileleni Simba, hata hivyo Yanga inakuwa juu kwa uwiano wa mabao ya kufunga kwani mpaka sasa ina mabao 10 na pointi 6, wakati Azam na Simba nazo zina pointi 6.

Mabao ya Yanga yamewekwa kimiani na Stepano Aziz Ki dakika ya 45, Kennedy Musonda dakika ya 54, Yao Kouasi dakika ya 64 na Maxi Nzengeli aliyefunga mawili dakika za 79 na 87.

Yanga inayonolewa na Muargentina Manuel Angel Gamondi bado inaendelea kusifika kwa kucheza kandanda safi


.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA