TUTAIUA AL AHLY KAMA KOMOROZINE- OKWI
Na Fikiri Salum Kama walivyotoa ahadi ya mabao kwenye mchezo wa ligi kuu bara kati yao na Ruvu Shooting ambapo wachezaji wa Yanga waliahidi kuifunga magoli mengi timu hiyo, ndivyo itakavyokuwa katika mchezo wa klabu bingwa barani Afrika kati ya mabingwa wa Tanzania bara na wawakilishi pekee katika michuano ya kimataifa Yanga dhidi ya mabingwa watetezi wa Afrika Al Ahly ya Misri. Yanga na Al Ahly ya Misri zitakutana kesho kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo wachezaji wa mabingwa hao wa bara wameahidi kuishushia kichapo kitakatifu Al Ahly kama waliofanyia Komorozine ya Comoro. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Emmanuel Okwi raia wa Uganda amesema ana usongo mkubwa katika michuano ya kimataifa na hasa mechi iliyo mbele yake, Okwi ametamba kutoka na magoli si zaidi ya mawili katika mechi hiyo kwani wapinzani wao ni timu ya kawaida kama nyingine, Naye Simon Msuva amedai Al Ahly ni timu ya kawaida na inafungika.