MASIKINI EMMANUEL OKWI! TFF YAMKANDAMIZA TENA KWENYE SAKATA JINGINE,IKIBAINIKA KUFUNGIWA MAISHA.
Sakata la uhamisho wa mshambuliaji Emmanuel Okwi limeanza kuwatafuna vigogo wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wakidai kushughulikia suala hilo kiushabiki badala ya kufuata taratibu.
Taarifa ya Ofisa habari wa TFF, Boniface Wambura jana ilisema kuwa kiongozi wa idara ya Takwimu, Sabri Mtulla analalamikiwa na shirikisho hilo kwa madai ya kuidanganya Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kuwa hakukuwa na pingamizi dhidi ya usajili wa Okwi huku akijua wazi kuwa jambo hilo si kweli.
“Kamati ilikutana mara ya kwanza, ikahoji kama kuna pingamizi lolote dhidi ya Okwi, lakini Mtulla alidanganya kuwa hakuna, kamati ilivyokutana kwa mara ya pili ikabaini pingamizi lilikuwepo, ila kiongozi huyo alificha wakati alijua wazi kuwa Simba walikuwa wameweka pingamizi wakipinga Okwi kusajiliwa na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili na nusu.
“Kwa mujibu wa kanuni, malalamiko hayo yamefikishwa kwenye Kamati ya Maadili ambayo itachunguza ili kujiridhisha kama yana msingi au la. Ikibaini kuwa kuna kesi ndipo walalamikiwa watafika mbele ya kamati hiyo kujibu mashtaka yao.”
Hata hivyo mtandao huu ulipomtafuta Mtulla kuhusiana na suala hilo alisema kwa kifupi: “Ofisi ndiyo inayonituhumu nimefanya udanganyifu, mimi nasubiri niitwe nitoe utetezi wangu, ili suala nalijua undani wake kuanzia mwanzo hadi lilipofika sasa, nitaweka wazi kila kitu, kwa kifupi wamelikoroga sasa wanatafuta pa kuangushia jumba bovu.”
Sinema ya usajili wa mshambuliaji huyo raia wa Uganda ilianza Mei 19, 2013 wakati Shirikisho la Soka nchini Uganda (Fufa) kupitia mtendaji wao mkuu, Edgar Watson lilipotuma barua kwa Shirikisho la soka la Tunisia likimwombea kibali Okwi kujiunga na kambi ya timu ya taifa (Uganda Cranes) iliyokuwa inajiandaa na michezo miwili dhidi ya Angola na Liberia kufuzu kushiriki Kombe la Dunia mwaka huu nchini Brazil.
Michezo hiyo ilikuwa ichezwe Juni 8 na 15 jijini Kampala na baada ya michezo hiyo Okwi hakurejea klabuni kwake, Etoile du Sahel.
Simba SC iliyomuuza kwa Etoile ilitaka kumrejesha kundini mwaka jana, lakini aliikwepa na kwenda SC Villa ya Uganda ili apate nafasi ya kucheza fainali za wachezaji wa ligi za ndani (Chan).
Okwi aliuzwa na Simba kwa Etoile kwa ada ya Dola 300,000 lakini Watunisia hao walishindwa kuwalipa Simba fedha za usajili huo kwa wakati, pia Okwi aligoma kuwachezea Waarabu hao kwa madai ya kushindwa kuheshimu makubaliano ya kimkataba.
Baada ya mgomo uliochukua miezi kadhaa SC Villa ambayo ndiyo iliyomkuza Okwi kabla ya kumuuza Simba, iliomba Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), kumruhusu arudi Uganda ili asipoteze kiwango chake na Fifa ilimruhusu kwa kumpa kibali cha miezi sita wakati suala lake likitatuliwa.