MAYWEATHER AFANYA KUFURU YA PESA.

BONDIA Floyd Mayweather amewaonyesha mamilioni ya wafuasi wake kwenye Twitter namna alivyosherehekea miaka 37 ya kuzaliwa kwake mwishoni mwa wiki kwa kupanda ndege binafsi na rafiki zake na timu ya walinzi wake kwenda kufanya 'kufuru'.


Mayweather, ambaye ameripotiwa kuachana na demu wake Shantel Jackson, alikuwa amezungukwa na marafiki kibao wa kike wakati akiangalia mechi ya mpira wa kikapu, Los Angeles Lakers ikiifunga Boston Celtics jana jioni.

Bingwa huyo mara nane wa dunia ambaye hajawahi kupoteza pambano anatarajiwa kupanda ulingoni Mei 3, lakini si kama ilivyotarajiwa awali angepigana na Muingereza, Amir Khan mjini Las Vegas baada ya kuwaambia wafuasi wake kwenye Twitter wapige kuraa apigane na nani kati ya Khan au Muargentina Marcos Maidana.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA