BRAZIL YAZINDUA MPANGO MPYA WA KUJILINDA
Brazil imetangaza kwamba
wameongeza maafisa wa kulinda usalama 70,000 zaidi watakao toa huduma za
usalama katika fainali ya Dimba la Kombe la Dunia mwaka huu.
Idadi iliyopendekezwa hapo mbeleni ya maafisa 100,000 .
Kwa ujumla maafisa wa usalama wapatao 170,000 watatumika katika miji 12 itakayoandaa mashindano hayo.
Jumatano wiki hii Rais wa Brazil Dilma Rouseff alisema kwamba jeshi litajumuishwa kwenye mpango huo dhabiti wa usalama iwapo kutaibuka wimbi lingine la maandamano.
Hatua hii inafuatia visa vya ghasia zilizoshuhudiwa katika miji tofauti tangu mwezi Juni mwaka uliyopita wakati Brazil ilipoandaa mchuano wa Kombe la Mashirika.
Mkuu wa Usalama wa Shrikisho la Soka Duniani FIFA amesema kuwa ana uhakika kwamba Brazil itaandaa mchuano wenye usalama.
Kati ya idadi hiyo ya maafisa wa usalama, 150,000 watachaguliwa kutoka katika vikosi vya Polisi na mashirika mengine ya usalama huku wengine 20,000 watatoa huduma usalama ndani ya viwanja vyote 12.
Vikosi vya jeshi la wanamaji pia litazindua mazoezi ya kwanza kwa matayarisho ya dimba la Kombe la Dunia.
Operesheni hiyo maalum ya kupambana na ghasia inawahusisha wanajeshi 20,000, meli 60 na ndege 15 za kivita.