UCHAGUZI TASWA KUMEKUCHA,PINTO,GEROGE JOHN KUCHUANA

WAOMBAJI 27 kati ya 28 wamerejesha fomu kuomba kuwania nafasi mbalimbali za uongozi kwenye uchaguzi wa Kamati mpya ya Utendaji ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) utakaofanyika Machi 2, 2014 jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TASWA, Boniface Wambura amesema leo kwamba, mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu hizo ilikuwa leo Alhamisi (Februari 27 mwaka huu) saa 9 alasiri.

Waliorejesha kwa nafasi ya ujumbe ni Arone Benedict Mpanduka, Elizabeth Rashid Mayemba, Emmanuel Augustino Muga, Hassan Maulid Bumbuli, Ibrahim Mkomwa Bakari, Masau Kuliga Bwire, Mbozi Ernest Katala, Mroki Timothy Mroki, Mussa Juma, Mwani Omary Nyangassa, Rehure Richard Nyaulawa, Salum Amiri Jaba, Tullo Stephen Chambo na Urick Chacha Maginga.


Mhazini Msaidizi ni Elius John Kambili, Zena Suleiman Chande wakati Mhazini Mkuu ni Shija Richard Shija na Mohamed Salim Mkangara.
Katibu Msaidizi ni Alfred Lucas Mapunda, Grace Aloyce Hoka na Ptarick Raymond Nyembera. Katibu Mkuu ni Amir Ally Mhando pekee.

Waombaji nafasi ya Makamu Mwenyekiti ni Egbert Emmanuel Mkoko, Maulid Baraka Kitenge na Mohamed Omary Masenga. Waliojitosa kwenye nafasi ya Mwenyekiti ni George John Ishabairu, Juma Abbas Pinto.
Mgombea mmoja ambaye licha ya kwamba alikuwa hakidhi sifa za kitaaluma, alichukua fomu za Uenyekiti, lakini amejishtukia na ni pekee ambaye hakurejesha fomu.

Katiba ya TASWA inaagiza mgombea awe angalau ana Cheti cha Mafunzo ya Uandishi wa Habari kwa nafasi za Ujumbe na nafasi nyingine, awe wa kiwango cha Diploma kuendelea, na mgombea aliyeingia mitini hana cheti cha mafunzo japo ya saa 24 ya Uandishi wa Habari.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA