PSG YAICHAKAZA BAYER LEVERKUSEN

Zlatan Ibrahimovic aifungia PSG dhidi ya Bayer Leverkusen
Zlatan Ibrahimovic alifunga mabao mawili na kuisaidia Paris St-Germain kusajili ushindi mkubwa wa mabao 4-0 dhidi ya Bayer Leverkusen katika mchuano wa ligi ya mabingwa barani Ulaya.

Blaise Matuidi ndiye aliyefungua mvua hiyo ya mabao alipotikisa wavu kunako dakika ya tatu ya ya kipindi cha kwanza na kumwacha kipa Bernd Leno amezubaa.


Ibrahimovic alifunga mkwaju wa adhabu na kuipa PSG bao la pili kunako dakika ya 39 .
Dakika tatu baadaye Ibrahimovic alifunga bao lake la pili kupitia mkwaju wa penalti, Spahic alipomzuia Ezequiel Lavezzi na refarii akaiadhibu Leverkusen.

Wafungaji bora Ligi ya Mabingwa 2013-14
  • Zlatan Ibrahimovic (PSG) 10
  • Cristiano Ronaldo (Real Madrid) 9
  • Lionel Messi (Barcelona) 7
  • Sergio Aguero (Man City) 6
  • Alvaro Negredo (Man City) 5
Mechi hiyo ilibakia kuwa ya nipe nikupe hadi muda wa lala salama ya kipindi cha pili hadi pale Yohan Cabaye alipocheka na wavu punde baada ya Emir Spahic kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kucheza visivyo.
Kutokana na mabao hayo mawili Ibrahimovic,sasa amempiku mchezaji bora duniani Cristiano Ronaldo kwenye orodha ya mfungaji bora katika msimu huu wa mwaka 2013-2014 wa ligi yenye kitita kikubwa zaidi barani ulaya akiwa na jumla ya mabao kumi.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA