JANUZAJ AITWA KOSOVO KUIVAA HAITI.

KINDA Adnan Januzaj amepigiwa simu na Naibu Waziri Mkuu wa Kosovo kuombwa aichezee mechi ya kwanza ya kimataifa nchi hiyo.

Behgjet Pacolli, bilionea mmiliki kampuni za ujenzi anayekadiriwa kuwa na utajiri wa Dola za Kimarekani Milioni 550, anajaribu kumshawishi Januzaj acheze dhidi ya Haiti mwezi ujao.

Januzaj, mwenye umri wa miaka 19, bado hajaamua acheze nchi gani soka ya kimataifa, lakini familia yake ilikuwa moja ya wanaharakati wa uhuru wa nchi hiyo.

Pamoja na hayo, Kosovo bado haijapata uanachama wa FIFA, wameruhusiwa kucheza mechi ya kwanza ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya Haiti mwezi ujao.


Januzaj alizaliwa mjini Brussels, Ubelgiji lakini kuna utata mkubwa juu ya mustakabali wake katika soka ya kimataifa.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI