NGASA AMFUNIKA OKWI YANGA.

BAADA ya mechi 20 za kuichezea klabu ya Yanga SC ya Dar es Salaam tangu arejee msimu huu, Mrisho Khalfan Ngassa amedhihirisha klabu hiyo haikukosea kumrejesha Jangwani.

Jumapili Ngassa alicheza mechi ya 20 tangu arejee Yanga SC msimu huu akitokea kwa mahasimu, Simba SC alikocheza msimu mmoja akitokea Azam FC, waliomtoa Jangwani mwaka 2009.

Ngassa alifunga mabao matatu katika ushindi wa 5-2 mjini Moroni, Comoro dhidi ya wenyeji, Komorozine katika mchezo wa marudiano Raundi ya Awali, Ligi ya Mabingwa Afrika.

Katika mechi hizo 20, Ngassa ametimiza mabao 15 na kuwapiku wachezaji kadhaa waliomtangulia, huku kukiwa kuna kila dalili atampiku Mrundi Didier Kavumbangu, mchezaji mwenye mabao mengi kati ya nyota waliojiunga na timu hiyo ndani ya misimu hii miwili.


WANAOONGOZA KWA MABAO YANGA

D. Kavumbangu Yanga   25 52
Mrisho Ngassa Yanga 15 20
Said Bahanuzi Yanga 14 39 
Simon Msuva Yanga 10 50
Nizar Khalfan Yanga 7 31
Emmanuel Okwi Yanga 3 4
Mbuyu Twite Yanga 3 52
Hussein Javu Yanga 2 9
(Orodha hii inawahusu wachezaji waliosajiliwa Yanga SC ndani ya misimu hii miwili tu)


Kavumbangu ameifungia Yanga mabao 25 katika mechi 52 za kirafiki na mashindano yote alizoichezea timu hiyo tangu ajiunge nayo msimu uliopita, moja likiwa la penalti.

Ngassa ambaye msimu uliopita akiwa Simba SC alifunga mabao saba ndani ya mechi 27, tayari amempiku Said Bahanuzi ambaye ameifungia Yanga mabao 14 katika mechi 39 ndani ya misimu miwili, yakiwemo matatu ya penalti.

Simon Msuva anashika nafasi ya nne kwa mabao yake 10 ndani ya mechi 50, Nizar Khalfan wa tano kwa mabao yake saba ndani ya mechi 31, nyingi akitokea benchi, Emmanuel Okwi wa sita kwa mabao yake matatu ndani ya mechi nne sawa na Mbuyu Twite aliyecheza mechi 52 wakati Hussein Javu amefunga mabao mawili ndani ya mechi tisa.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA