Ruka hadi kwenye maudhui makuu

TUTAIUA AL AHLY KAMA KOMOROZINE- OKWI

Na Fikiri Salum

Kama walivyotoa ahadi ya mabao kwenye mchezo wa ligi kuu bara kati yao na Ruvu Shooting ambapo wachezaji wa Yanga waliahidi kuifunga magoli mengi timu hiyo, ndivyo itakavyokuwa katika mchezo wa klabu bingwa barani Afrika kati ya mabingwa wa Tanzania bara na wawakilishi pekee katika michuano ya kimataifa Yanga dhidi ya mabingwa watetezi wa Afrika Al Ahly ya Misri.

Yanga na Al Ahly ya Misri zitakutana kesho kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ambapo wachezaji wa mabingwa hao wa bara wameahidi kuishushia kichapo kitakatifu Al Ahly kama waliofanyia Komorozine ya Comoro.

Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Emmanuel Okwi raia wa Uganda amesema ana usongo mkubwa katika michuano ya kimataifa na hasa mechi iliyo mbele yake, Okwi ametamba kutoka na magoli si zaidi ya mawili katika mechi hiyo kwani wapinzani wao ni timu ya kawaida kama nyingine, Naye Simon Msuva amedai Al Ahly ni timu ya kawaida na inafungika.



'Katika mchezo huo lengo langu ni kupeleka mashambulizi mengi langoni mwao na ikiwezekana na mimi nifunge moja au mawili, nawaambia mashabiki wa Yanga waje washuhudie kalamu ya magoli uwanja wa Taifa', alisema Msuva ambaye amekuwa katika kiwango cha juu siku za hivi karibuni.

Mrisho Ngasa ambaye anaongoza kwa magoli barani Afrika ametamba kutoka na goli zake mbili ama tatu katika mchezo huo huku akiahidi mvua ya magoli kuendelea, 'Tutashinda tu katika mechi hiyo, Yanga hii si timu ya kuichezea ni moto wa kuotea mbali tena tutafunga mengi, ni msimu wetu kusonga mbele', alisisitiza Ngasa.

Kocha msaidizi wa Yanga Charles Boniface Mkwasa amesema Al Ahly ni timu ya kawaida sana na ameiona ilipocheza na Sfaxien katika fainali ya Super Cup, 'Ni timu ya kawaida na inawezekana tukaifunga, kuhusu goli ngapi hiyo ni mipango ya mungu lakini lazima tuwafunge, nimezijua mbinu zao na tutazifanyia kazi', aliongeza Mkwasa.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa