ENGLAND YAAJIRI MWANASAIKOLOJIA
Kocha wa Uingereza Roy Hodgson amesajili huduma za daktari wa akili ama ilikuwasaidia wachezaji wake kuimarisha uwezo wao wa
kupiga penalti katika kampeini yake ya fainali za kombe la dunia litakaloandaliwa huko Brazil baadaye mwaka huu.Hodgson tayari amemsajili afisa wa shirikisho la uendeshaji baiskeli Sir Dave Brailsford kusaili kikosi chake.
Brailsford anasifika kwa kuongoza ufanisi wa timu ya mbio za uendashi baiskeli ya Uingereza na Hogdson amemwalika kuzungumza na wachezaji
kabla ya mechi ya ya kujipima nguvu dhidi ya Peru .
Kutokana na rekodi mbaya ya kupiga mikwaju Hogson sasa anafikiria kumwajiri mwanasaikolojia kwa niya ya kuwanoa kiakili wachezaji wake.
Uingereza imeshinda mechi moja pekee dhidi ya Uhispania (1996) kati ya saba iliyoamuliwa kwa mikwaju ya penalti huku takwimu zikionyesha kuwa
kati ya penalti 35 zilizopigwa Uingereza ilifunga mikwaju 23 pekee.
Uingereza ilishindwa na Italia katika mechi yao ya kwanza chini ya ukufunzi wake Hogson kwa mikwaju ya penalti .