MBEYA CITY WAPIGA KAMBI MOMBASA KUIUA COASTAL UNION KESHO
Na Salum Fikiri Jr
Kikosi cha Mbeya City kimeweka kambini jijini Mombasa, Kenya kwa ajili ya mechi yao ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya Coastal Union itakayochezwa Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga kesho.
Msemaji wa Mbeya City, Fred Jackson alisema jana kuwa, kikosi chao kinachonolewa na kocha mzawa, Juma Mwambusi kitakuwa kikijifua jijini Mombasa hadi kesho asubuhi kitakaposafiri kwa basi kwenda jijini Tanga kuwakabili Coastal Union jioni.
"Tulianza safari yetu kuelekea Kenya jana (juzi), tumelala Dar es Salaam. Asubuhi hii tunaunganisha ndege kwenda Mombasa ambako timu itakaa hadi Jumamosi asubuhi," alisema Jackson.
Alisema lengo la kambi hiyo ni kuwafanya wachezaji wao wazoee hali ya hewa ya Mombasa ambayo inawiana na Tanga ambako watawakabili mabingwa wa Tanzania Bara 1988, Coastal Union wanaonolewa na kocha Mganda Yusuph Chipo baada ya kuachana na Hemed Morocco mzunguko wa kwanza.
Wababe hao wa ligi kuu kutoka jijini Mbeya wanakamata nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo wakiwa na pointi 35 sawa na mabingwa watetezi Yanga walioko nafasi ya pili.
Coastal iliyokuwa imeweka kambi mjini Muscat, Oman kwa ajili ya mzunguko wa pili wa ligi iko nafasi ya saba ikiwa ni baada ya kukusanya pointi 22 katika mechi 18.
Waliokuwa wawakilishi wa Tanzania Bara katika mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika, Azam FC wanakamata usukani wakiwa na pointi 36 baada ya kucheza mechi 16 sawa na Yanga.