FLAMINI AZICHAPA KAVUKAVU NA WILSHERE

KIUNGO Jack Wilshere ameposti picha inayomuonyesha akipigana na mchezaji mwenzake Mathieu Flamini baada ya mazoezi jana kwenye basi la timu.

Viungo hao wawili walipigwa picha wakionekana kutofautiana kwenye mazoezi ya timu hiyo saa 24 kabla ya Arsenal kuwakaribisha Black Cats katika mchezo wa Ligi Kuu.

Nipishe: Jack Wilshere amehusishwa na kutofautiana na mchezaji mwenzake Mathieu Flamini kwenye mazoezi ya Arsenal jana na Bacary Sagna anaonekana kwenda kusuluhisha.

Sakata la wachezaji hao wawili wa Arsenal linakuja siku kadhaa baada ya Flamini kutaka kugombana hadharani na Mesut Ozil wakifungwa mabao 2-0 na Bayern Munich Uwanja wa Emirates.


Kiungo huyo Mfaransa alimvaa Ozil akimtuhumu mchezaji huyo aliyenunuliwa kwa Pauni Milioni 42.5 kutojituma kwenye mechi hiyo.
Arsenal wanarejea uwanjani leo kumenyana na Sunderland katika Ligi Kuu ya England wakitoka kutoa sare na Manchester United na kufungwa na Liverpool katika mechi zao mbili zilizopita.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA