MKOLA MAN ATOBOA SIRI YA KUJIUNGA FREEMASON, ADAI WASANII 20 TANZANIA WAMO KWENYE DINI HIYO.

Na Prince Hoza

TANGIA ilipoanza kupa kufahamika miongoni mwa wanadamu dini ya kishetani ya freemason imeanza kupata wanachama wengi, idadi kubwa ya watu hasa katika bara la Afrika imezidi kuongezeka.

Nchini Tanzania kundi kubwa la vijana wanaoamini ukijiunga na dini hiyo ya kishetani unafanikiwa kimaisha, dini hiyo iliyoingia nchini miaka michache iliyopita ikitokea nchi jirani za Kenya na Uganda ambapo ndipo ilipoanza kupokelewa na kusambaa katika mikoa ya kaskazini mwa Tanzania.

Lakini freemason Lakini freemason ilikuwepo tangia kuanzishwa kwa kanisa la Roma katoliki, chimbuko la imani hiyo inatokana na watoto wawili wa nabii Nuhu (Noa) Mashindano ya kwanza kufanyika duniani ya Olimpiki ni sehemu ya kusambaa kwa dini hiyo ya kishetani ambapo waumini wake hudiriki kusali wakiwa uchi.

Baada ya kutapakaa sehemu mbalimbali duniani freemason iliingia nchini na baadaye ilianza kukubalika, Freemason uligeuka mtandao mkubwa na watu mbalimbali walijiunga kwa malengo  ya kufanikiwa haraka, utajiri wa mali, fedha na umaarufu vimetajwa kama sehemu iliyosababisha watu wengi kuikimbilia imani hiyo ili kuweza kubadili maisha yao na hatimaye kuwa watu wanaoheshimika sana.


Watu mbalimbali waliamini ukijiunga na dini hiyo utafanikiwa haraka, wanasiasa, wanamichezo, wanamuziki na wafanyakazi wengine ni miongoni mwa watu waliojiunga katika imani hiyo, pia wapo wapo viongozi wa dini mbalimbali na waganga wa kienyeji ambao ni wafuasi wa imani hiyo inayoelekea kuitawala dunia.

Freemason inaelekea kuitawala dunia kwa sababu inasifika kwa kutakatisha nyota za watu bila kujali wanatoka kundi lipi, taarifa mbalimbali zilizowahi kutolewa huko nyuma zinaonyesha kuwa wapo watu maarufu nchini wamo katika imani hiyo.

Lakini wapo watu wanaohiofia imani hiyo kutokana na na miujiza yake, inasemekana mtu anayejiunga na dini hiyo anabadilika ghafla na kuondoa utofauti wake na mwanzo, watu wengi wanaotajwa kuwemo kwenye dini hiyo ya kishetani wameonekana tofauti na mwanzo hasa kimtazamo.

Wapo wanamuziki ambao hapo nyuma hawakuwa na mafanikio yoyote na wala tungo zao zilikosa mashiko, lakini walipohusishwa kujiunga na imani hiyo muziki wao umekuwa ukipendwa na hata anaposimama jukwaani watu wengi uhudhuria kiasi kwamba anajikusanyia fedha nyingi.

Hofu nyingine ni ile inayotokana na masharti ya kujiunga na imani hiyo, damu inatajwa kama ada ya kujiunga, huku ikihusishwa na kifo kwa mtu anayependwa ambaye anakuwa kama sadaka kwa mungu wa imani hiyo.

Mtu anayejiunga na dini hiyo akibainika anaogopwa sana na jamii iliyomzunguka kiasi kwamba anatengwa, kwanza utajiri na umaarufu wa kushangaza ni moja kati ya vitu vinavyopelekea kuzusha hofu lakini sadaka ya kumtoa mwanadamu mwenzio ndio inayopelekea kutengwa na jamii ikiwemo ndugu.

Christopher Mhenga wengi humfahamu kwa jina la Mkola Man mzaliwa wa Hale mkoani Tanga anatajwa kama muumini wa dini hiyo ya kishetani, Mkola Man ni mwanamuziki wa kizazi kipya maarufu kama bongofleva ambaye hivi karibuni aliachia wimbo wake mpya uitwao Kilevi changu.

Wimbo huo umeanza kufanya vizuri kwenye vituo vya redio jijini Tanga na mikoa jirani na sasa hivi amepata mialiko kadhaa ikiwemo katika nchi za Kenya, Rwanda na Burundi, Mtandao wa mambouwanjani.blogspot.com uliwahi kuandika habari zake kuwa amejiunga na dini hiyo ya kishetani.

Mwandishi wa makala hii alifunga safari hadi Hale anapoishi msanii huyo na kufanya naye mahojiano, Mkola Man alimthibitishia mwandishi kuwa yeye ni mfuasi wa freemason lakini tofauti na watu wanavyoielezea.

Freemason ni dini kama nyingine, inaongozwa na mchungaji na pia inatoa fulsa kwa waumini wake kutafuta riziki tena kwa bidii ili kupeleka sadaka, yaani kama zilivodini nyingine zote zina sadaka n,k alisema Mkola Man.

'Kuhusu kutoa damu, hilo si geni hata dini nyingine zinafanya hivyo, biashara ya damu nadhani ilishamili hapa nchini, watu walikua wakiuawa kwa kunyonywa damu na kisha maiti zao kugongwa muhuri, hivyo hata ilipokomeshwa benki ya damu ya dunia bado inaendelea kukusanya  damu', aliongeza.

'Unafikiri zile damu zinapelekwa wapi? ni kwa ajili ya kuwachangia watu wenye upungufu wa damu, wakristo huchangia damu na kuzipeleka mahospitalini kwa ajili ya wenye mapungufu ya damu, na waislamu hufanya hivyo hivyo, na sisi freemason tunatoa damu kwa ajili ya wagonjwa iweje tuonekane tuko fotauti! alishangaa Mkola Man.

KUHUSU IMANI YA KIFO: 'Kweli hata vitabu vitakatifu vya mwenyezi mungu kama biblia na kur'aan zinaelezea kifo, kifo ni sawa na sadaka na ndio maana mtu akifa tunatanguliza shukrani, pia tunasoma wosia kwa familia, neno mungu amempenda kiumbe chake hutawala;, alisisitiza.

Aidha Mkola Man alielezea jinsi yeye alivyoshawishika kujiunga na dini hiyo, 'kikubwa mimi nimefuata Upako, freemason ni dini ya kweli inayomwamini mungu tofauti na dini nyingine zinazoaminika machoni mwa watu', aliendelea kusema.

'Sidhani kama umewahi kusikia mtu aliyemo kwenye imani hii anafanya matendo mabaya kama kushiriki uchawi, freemason ni watu wema tena wanaharakati katika maisha, ukijiunga katika imani hii utafanikiwa kimaisha', alisema.

'Kwanza umasikini ni dhambi freemason inaamini hivyo, ndio maana ukiwa masikini unaweza kumkufuru mungu, utaona kwanini amewapa wale na amekunyima wewe, imani hii inampa muumini wake maisha bora na ya kujiamini', aliendelea.

'Muziki umenifanya nijitumbukize kwenye dini hii kwa sababu ninacho kipaji lakini sijapata mafanikio yeyote, hapo mwanzo niliwahi kutoa wimbo wangu wa kwanza usemao Utajiri hewa, ambapo freemason walinifuata na kudai nimewatukana, na nyimbo yangu hiyo itakuwa hewa, wakanipa wazo la kuandika nyimbo nyingine ndio nikaitoa Mr Mapesa na kweli ilipata mafanikio hadi kuingizwa kwenye Top Ten za redio mbalimbali nchini', aliongeza.

Nilipojiunga na freemason nikapewa ushauri na jinsi ya kufanikiwa kwamba kunahitaji subira, kweli niliamini na nikaombewa na mchungaji kisha nikatakiwa kuchangia damu ambapo nilipasuliwa kwenye kidole changu cha mkono wa kushoto na kutobolewa yaani kamaunavyopima malaria', aliongeza.

Baadaye nikaambiwa sala niliyoombewa na mchungaji ina Upako hivyo maisha yangu yatanyooka, nilifanikiwa kuingia tena studio kutengeneza wimbo wangu mpya wa Kilevi changu ambao unafanya vizuri kwa sasa kwenye stesheni za redio', alisisitiza.

'Niko mbioni kuutolea video mara baada ya kurejea nchini nikitokea zangu katika nchi za Kenya, Burundi na Rwanda ambapo nitakuwa na maonyesho ya kimuziki, nimealikwana nitaenda kuwapa burudani mashabikji wangu wa huko', aliendelea.

Nyota yangu inang'ara baada ya kujiunga na freemason, ingawa familia yangu hainielewi lakini nikiupata utajiri yote yatakwisha, kuwepo kwangu katika dini hii ina maana sitazeeka, sitaugua hovyo na nitaogopeka na jamii ila kinga yangu ni kubwa lakini kifo changu kitashangaza', alizidi kufafanua.

Aidha Mkola Man alisimulia jinsi alivyojiunga kwa mara ya kwanza ambapo katika daftari la maudhurio alikutana na majina 20 ya wasanii maarufu hapa nchini na majina 30 ya wanasiasa huku watu wengine maarufu wakiwemo viongozi wa dini mbalimbali nchini, ITAENDELEA JUMAMOSI IJAYO.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA