PISTORIUS AJUTIA KIFO CHA MPENZI WAKE

Oscar Pistorius
DUNIA leo inaadhimisha siku ya wapendanao yaani Valentine Day, Mwanariadha wa Afrika Kusini Oscar Pistorius, amezungumzia masikitiko na majuto yake kuhusu mauaji ya aliyekuwa mpenzi wake Reeva Steenkamp, mwaka mmoja uliopita.

Katika taarifa kwa mtandao wake, alisema: ''Kumpoteza Reeva kulinipa huzuni mkubwa sana siku hiyo na nitaubeba maisha yangu yote.''

Kesi ya mauaji dhidi ya Pistorius inatarajiwa kuanza mjini Pretoria mnamo mwezi Machi.
Oscar anasema kuwa alimpiga risasi Reeva kwa bahati mbaya baada ya kudhani kuwa alikuwa jambazi ndani ya nyumba yake alipompiga risasi kupitia mlango wa bafu yake mwaka 2013.
Mwendesha mkuu wa mashitaka anadai kuwa mauaji hayo yalikuwa ya kupangwa baada ya wawili hao kuzozana.


Huenda akafungwa jela maisha ikiwa atapatikana na hatia.

Nini kilitendeka usiku huo?

Kukamatwa kwa Pistorius mwaka jana kuliwashangaza wengi sana nchini Afrika Kusini na duniani kote hasa kwa wale waliomuona kama mwanamichezo mahiri na ambaye ni kioo cha jamii hasa baada ya kuteta kwa miaka mingi na kutaka aruhusiwe kushiriki michezo.

Mwanamichezo huyo mwenye umri wa miaka 27, alishinda medali ya dhahabu katika michezo ya Olimpiki ya walevamu mwaka 2012 na pia kwenye michezo ya Olimpiki.
Mepama wiki hii, familia ya Reeva ilisema kuwa mamake June atahudhuria kesi dhidi ya Pistorius ambayo inatarajiwa kuanza tarehe 3 mwezi Machi.

Reeva Steenkamp, alikuwa mwanamitindo mwenye umri wa miaka 29. Alipigwa risasi mara tatu alipokuwa bafuni nyumbani mwa Pistorius tarehe 14 Februari 2013.

Pistorius alisema kuwa alidhani mtu aliyeingia nyumbani kwake alikuwa jambazi na anakana madai kuwa walikosana na Reeva masaa za asubuhi siku hiyo kabla ya kumpiga risasi.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA