MAKALA; WIMBI HILI LA VIGOGO WA SIMBA NA YANGA KUJAZANA TFF LINAASHIRIA NINI?
Na Prince Hoza
WAKATI Watanzania wakijiandaa kutimiza miaka 53 ya muungano huku kukiwa na mafanikio hafifu kwenye ekta muhimu, upande wa michezo nao si lolote, Kilio kikubwa ni ukosefu wa viwanja pamoja na uduni wa kiwango cha soka kinachoonyeshwa na timu ya taifa, Taifa Stars.
Taifa Stars imeonyesha kuwakera wadau wa soka nchini na kuamua kuhamishia mapenzi yao kwa timu za mataifa mengine, uzalendo umetoweka kabisa, mwaka 2006 rais wa TFF wakati huo Leodegar Tenga alitangaza mikakati kabambe ya kurejesha hamasa ya soka nchini.
Tenga alitangaza kutengeneza misingi imara ya soka nchini, jitihada za Tenga ziliungwa mkono na rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe Jakaya Mrisho Kikwete.
Kikwete aliahidi kumlipa mshahara mwalimu wa timu ya taifa, Taifa Stars kupitia serikali yake, ahadi hiyo pia aliitoa kwa vyama vya michezo mingine.TFF ilishauriwa kutafuta kocha wa kigeni na ilibahatika kumleta Mbrazil Marcio Maximo, Maximo alianza kufundisha soka nchini na kufanikiwa kutengeneza timu ya taifa iliyobadilisha mwonekano wa soka nchini.
Timu hiyo ilitoa ushindani na kufanikiwa kufuzu kwa mara ya kwanza fainali za mataifa Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani maarufu CHAN.
Imani ya Watanzania ilianza kurejea ambapo sasa wapenzi wa soka walianza kuiunga mkono timu yao huku uzalendo ukiwaingia kwa kuvaa jezi ya taifa lao, mwenendo wa timu ya taifa ulianza kuelekea kubaya hasa baada ya kushindwa kuchukua ubingwa kwenye michuano ya CECAFA.
Hapo ndipo kelele zilipoanza hasa zikielekezwa kwa kocha wa timu ya taifa Marcio Maximo, Maximo aliandamwa kutokana na uteuzi wake wa kikosi ikidaiwa anapendelea zaidi wachezaji wa Simba na Yanga huku timu hizo vigogo zikionekana tatizo kwenye maendeleo ya soka nchini.
Simba na Yanga zimeonekana 'Problem' kwenye soka la Tanzania kiasi kwamba wadau wa soka walipendekeza ipatikane timu ya taifa inayotokana na mchanganyiko wa wachezaji huku Simba na Yanga zikitoa mchezaji mmoja mmoja.Lakini cha maajabu zaidi zikicheza Simba na Yanga idadi kubwa ya mashabiki hujitokeza kuliko zinapocheza timu nyingine, TFF iliamua kuachana na Maximo na ikampa ajira 'Kibabu' Jan Poulsen raia wa Denmark.
Mambo yakaonekana yaleyale, Jan Poulsen hakudumu sana na akatimuliwa, ajira ikaelekezwa kwa Mdenmark mwenzake ambaye alikuwa kocha wa timu ya taifa ya vijana Kim Poulsen, Kim alionekana mwarobaini wa soka la Tanzania kutokana na falsafa yake ya kupendelea zaidi vijana wadogo.
Utawala wa Tenga uliondoka rasmi madarakani na Jamal Malinzi ndiye bosi mpya wa soka la Tanzania. ,Malinzi amekuja na nguvu mpya na ameahidi kuendeleza soka na ikiwezekana timu ya taifa itafuzu fainali zijazo za mataifa Afrika.
Bila shaka wadau wa soka wameridhishwa na kauli ya Malinzi na wakiamini mafanikio yatakuwepo, watu wanataka ushindi na si siasa kama ilivyozoeleka katika siku za nyuma kwa viongozi wetu wa soka.
Usimba na Uyanga umetajwa kama adui wa soka la Tanzania na kuna wengine wameenda mbali zaidi ambapo wamefikia hatua ya kuziombea dua baya timu hizo kongwe nchini ili zife.
Wanataka kufananisha na Kenya ambapo walifanikiwa kuziua makali timu hasimu za Gor Mahia na AFC Leopard's, timu hizo zilisababisha soka la Kenya kupoteza msisimko na kufikia kuondoa mashabiki viwanjani.
Mtindo huo uliotumika Kenya wa kuziua Gor Mahia na AFC Leopard's ulitaka kutumika hapa nchini, Azam FC na Mbeya City zinapigana vikali kuumaliza ufalme wa Simba na Yanga.
Azam FC takribani misimu miwili imekamata nafasi mbili za juu na ikiwakilisha taifa, huku Simba na Yanga zikipokezana ubingwa na ile inayoshindwa hujikuta katika nafasi ya tatu.Msimu huu Azam FC inaongoza ligi hadi sasa na Yanga ikishika nafasi ya pili wakati vijana wa Mbeya City wakikamata nafasi ya tatu na Simba ikishika nafasi ya nne, uwiano huo unaelekea kuzipunguza makali Simba na Yanga ambazo zilikuwa zikitawala nafasi ya kwanza na ya pili kwa miaka nenda rudi, ipo siku zitaanguka kama Gor Mahia au AFC Leopard's.
Chakushangaza ni pale rais wa shirikisho la kandanda nchini TFF Jamal Malinzi alipoteua wajumbe katika kamati mbalimbali ndani ya shirikisho hilo huku wengi wao ni vigogo wa Simba na Yanga.
Wimbi la vigogo wa Simba na Yanga limezidi kuwa kubwa, sipati picha uwepo wao ndani ya TFF kama unaweza kuleta mabadiliko ya kweli ya soka la Tanzania au wanataka kulinda maslahi ya vilabu vyao.
Nimeshindwa kuelewa umuhimu wao kwani kilio cha wengi kilikuwa kwa Simba na Yanga kuwa ndiyo wanaozorotesha maendeleo ya soka la Tanzania, hata rais Jakaya Mrisho Kikwete aliwahi kuziponda timu hizo kwani zimezidiwa ujanja na timu changa ya Azam FC.
Kikwete aliziponda timu hizo wakati alipoalikwa na klabu ya Azam katika uzinduzi wake wa uwanja wa kisasa uliopo Mbagala Chamanzi nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, wasiwasi wangu kwa kamati za TFF zilizojaa vigogo wa Simba na Yanga zinaweza kuzorotesha maendeleo ya timu zinazotishia uwepo wao kama Azam FC na Mbeya City.
Timu hizi za Simba na Yanga hazipendi kufungwa, hivi karibuni Simba ilifungwa na JKT Mgambo ya Tanga ambapo uongozi wa Simba ulisikika ukilaani kitendo cha Mgambo kucheza butua butua ili kulinda goli lao lisirudi.
Kauli hiyo ilitolewa na mwenyekiti wa Simba Alhaj Ismail Aden Rage pale alipoamua kuwaita wachezaji wake wote pamoja na kocha jijini Dar es Salaam ili kujua nini kimepelekea timu hiyo kushindwa kuibuka na ushindi katika mechi zake mbili dhidi ya Mtibwa Sugar na Mgambo JKT.
Mechi hizo zilizochezwa nje ya Dar es Salaam ilishuhudia Simba ikienda sare ya kufungana 1-1 na Mtibwa Sugar katika uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro kabla haijakubali kipigo cha bao 1-0
dhidi ya Mgambo Mgambo JKT katika uwanja wa CCM Mkwakwani jijini Tanga.Simba ilikuwa ielekee jijini Mbeya moja kwa moja kuikabili Mbeya City, lakini mwenyekiti wake Ismail Aden Rage aliirejesha jijini Dar es Salaam na kufanya mazungumzo na wachezaji, Rage hakuamini kama Mgambo JKT inaweza kuifunga Simba na ndio maana alitaka kujua kama kuna kamgomo baridi kati ya wachezaji na kocha wao Mcrotia Zdravko Logarusic.
Hivi karibuni yalienea maneno kuwa wachezaji wa Simba wanacheza chini ya kiwango kwa lengo la kumuonyesha kwa vitendo kocha wao kuwa hawapendi kutukanwa.Baadaye Afisa habari wa timu hiyo Asha Muhaji alikanusha uvumi huo kupitia vyombo vya habari, ila kitendo cha Rage kuwaita wachezaji pamoja na kocha wao na kuzungumza nao katika vipindi tofauti kuliashiria kuwepo dosari katika timu hiyo.
Rage alinichekesha zaidi pale aliposema Mgambo JKT ilitumia mbinu za Jose Mourinho wa Chelsea anayetumia mtindo wa 'kupaki-basi', Mgambo walipopata bao moja hawakutaka kutafuta lingine na waliamua kulinda lango lao, alisikika Rage.
Ni dhahiri vigogo wa Simba na Yanga waliopo TFF watafanya kazi kubwa kuhakikisha maslahi ya timu zao yanalindwa, tusitegemee mabadiliko yoyote kupitia kamati hizo zenye sura ya Uyanga na Usimba.
Tunawafahamu sana na ndio maana tunaingiwa na hofu juu ya kuwepo kwao katika chombo hicho cha kusimamia mpira wa miguu hapa nchini, vigogo hao wenyewe wanajiita 'wazee wa fitina za mpira' Fitina gani hizo? jibu unalo.