UHURU SELEMAN AINYIMA UBINGWA SIMBA
Uhuru Suleiman amesema timu yake ya Simba ina mazingira magumu ya kutwaa
ubingwa kutokana na ushindani mkali iliopo kwenye ligi kuu ya Bara
ugumu uliopo katika duru la pili.
Lakini, kiungo huyo amesema, Simba bado ina nafasi ya kutwaa taji hilo kama itarekebisha makosa yaliyojitokeza nyuma na kufanya vizuri katika mechi zilizosalia.
Akizungumza na Nipashe katikati ya wiki, Uhuru ambaye hakuambatana na Simba jijini Mbeya ambako ilitoka sare ya 1-1 na Mbeya City Jumamosi iliyopita alisema ligi imekuwa gumu kutokana na timu kukamiana na ndiyo maana timu yake haifanyi vema.
"Ligi katika duru la pili imekuwa ngumu mno," alisema Uhuru nyota wa zamani wa Mtibwa Sugar na Coastal Union.
"Timu zinakamia na zinafukuzia pointi tatu."
Hata hivyo alisema pamoja na Simba kuonekana kuyumba katika mechi zake za karibuni, bado ina nafasi ya kuwa bingwa kwa sababu kuna mechi nyingi kabla ya msimu kufungwa.
Simba iliyopoteza pointi saba katika mechi zake tatu zilizopita kwa kupata sare mbili dhidi ya Mtibwa Sugar na Mbeya City na kulala kwa Mgambo JKT ipo nafasi ya nne kwenye msimamo, ikiwa pointi nne nyuma ya viongozi Azam wenye mechi mbili mkononi juu.
Mabingwa hao wa zamani kesho wataikabili JKT Ruvu iliyo katika nafasi za katikati za msimamo na ambayo mwalimu wake mpya kocha msaidizi wa zamani wa Yanga, Fred Felix 'Minziro' alipokelewa na kipigo cha 6-0 kutoka kwa Prisons katikati ya wiki.