REAL MADRID HAIKAMATIKI HISPANIA.

TIMU ya Atletico Madrid jana ilikula ngwala katika mbio zake za ubingwa wa La Liga baada ya kuchapwa mabao 3-0 na Osasuna, hivyo kuwaacha Real Madrid wajinafasi kileleni kwa pointi tatu zaidi.

Mabingwa Barcelona na vinara Real walilazimishwa sare kwenye Uwanja wa Osasuna, El Sadar mjini Pamplona mapema msimu huu na Atletico ikadondoka jana.


Alvaro Cejudo alifunga bao la kwanza dakika ya sita wakati makosa ya beki wa pembeni, Juanfran yalimruhusu Emiliano Armenteros kufunga bao la pili dakika ya 21 kabla ya Roberto Torres kufunga la tatu dakika ya 42. Atletico inabaki na pointi 60 sawa na Barcelona iliyo katika nafasi ya pili kwa wastani mzuri wa mabao, wakati Real pointi 63 juu yao.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA