TFF KUMRUHUSU OKWI KUKIPIGA YANGA.
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesema linajipanga kulipigia simu Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kusaka ufafanuzi wa uhalali wa usajili wa mshambuliaji Emmanuel Okwi kwa klabu ya Yanga.
Januari 22 mwaka huu ikiwa ni siku mbili tu kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF ilisimamisha usajili wa Mganda huyo katika klabu ya Yanga wakati likisubiri ufafanuzi Fifa.
Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura amesema jana mchana jijini hapa kuwa baada ya kusubiri kwa muda mrefu pasipo kupewa ufafanuzi wowote, wameamua kulitwangia simu shirikisho hilo la kimataifa.
"Suala la Okwi bado halijapata ufumbuzi kwa sababu hatujajibiwa chochote na Fifa mpaka sasa, kwa kuwa tumeshaandikia barua kuwakumbusha tunahitaji ufafanuzi na hawajatujibu, itabidi tuwapigie simu," amesema Wambura.
"Fifa ni taasisi kubwa, pengine wanahitaji kukumbushwa kuhusu suala hilo ndiyo maana tumeamua tuwapigie simu ili tujue limefikia wapi na ikiwezekana watu au kamati inayolishughulikia," amesema zaidi Wambura bila kueleza siku ambayo shirikisho hilo litapiga simu Fifa.
Okwi, ambaye aliingia mgogoro na klabu yake ya Etoile du Sahel (ESS) ya Tunisia aliruhusiwa na Fifa kuchezea SC Villa kwa kibali maalumu (provisional permit) cha miezi sita ili kulinda kiwango chake wakati suala lake dhidi ya klabu hiyo ya Tunisia likishughulikiwa na shirikisho hilo la kimataifa.
Lakini, SC Villa ilimuuza mchezaji huyo wa zamani wa Simba kwa mkataba wa miaka miwili na nusu kwa Yanga Desemba mwaka jana akiwa ametumikia miezi minne kati ya sita aliyoruhusiwa na Fifa kukaa katika klabu hiyo ya Uganda.
Wakati hali hiyo ikiendelea katia ya Yanga na TFF, klabu ya Simba nayo haijalipwa dola za Marekani 300,000 (Sh. milioni 480) za mauzo ya mshambuliaji huyo hatari kwa kufumania nyavu kwa ESS tangu Januari mwaka jana ilipowauzia wawakilishi hao wa Tunisia katika mashindano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.