TUTU AMSIHI MUSEVENI ASISAINI MUSWADA WA MASHOGA
Askofu mstaafu wa Cape Town,
Desmond Tutu, amemsihi Rais Museveni wa Uganda asitie saini mswada
ulioleta utatanishi kuhusu wapenzi wa jinsia moja.
Desmond Tutu alisema haistahiki kuwa na ubaguzi kama huo, na alitoa mifano ya mfumo wa zamani wa ubaguzi wa rangi uliokuwako Afrika Kusini na ubaguzi wa Wa-Nazi wa Ujerumani.
Alisema hiyo ni mifano mibaya kabisa.
Awali mswada wa Uganda ulipendekeza kifo kwa vitendo vya kulawiti na baadae kubadilishwa kuwa adhabu ya kifungo.