LIVERPOOL SI LOLOTE KWA ARSENAL, YADUWAZWA 2-1

BAO la Alex Oxlade-Chamberlain na pasi ya bao vimetoa mchango mzuri kwa Arsenal kutinga Raundi ya sita ya Kombe la FA baada ya kuifunga Liverpool mabao 2-1 Uwanja wa Emirates.

Kiungo huyo kinda wa England alifunga bao la kwanza dakika ya 16 akimalizia pasi ya Lukas Podolski, aliyefunga bao la pili dakika ya 47.
Refa Howard Webb aliwapa penalti Liverpool baada ya Podolski kumchezea faulo Luis Suarez, na Steven Gerrard akaenda kufunga dakika ya 59.


Pamoja na hayo, Webb alimezea penalti nyingine ya Liverpool baada ya Oxlade-Chamberlain kumuangusha Suarez kwenye eneo la hatari.

Liverpool ilitawala mchezo na kutengeneza nafasi nyingi za kusawazisha, lakini mwisho wa mchezo, Arsenal walifanikiwa kulipa kisasi cha kufungwa mabao 5-1 Uwanja wa Anfield katika Ligi Kuu.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA