MAKALA. YANGA IKAFIE UWANJANI NA KUPINDUA MEZA ALGERIA
WAWAKILISHI wa Afrika mashariki na kati Dar Young Africans, maarufu Yanga SC ilianza vibaya kwenye mchezo wake wa kwanza wa fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika, baada ya kufungwa mabao 2-1 katika uwanja wake wa nyumbani wa Mkapa uliopo jijini Dar es Salaam. Yanga ilipokea kipigo hicho kutoka kwa USM Alger ya Algeria, hivyo itakuwa na kazi ngumu kwenye mchezo wa marudiano utakaofanyika Jumamosi ijayo mjini Algiers nchini Algeria. Mimi binafsi sina wasiwasi na Yanga hasa inapofikia kwenye hatua kama hii ambapo Yanga inahitaji kufia uwanjani na mwisho wa siku kuibuka na ushindi ikiwezekana wa mabao 2-0 au zaidi. Yanga inapewa sapoti kubwa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan ambaye amejitolea ndege ya serikali kusafirisha wachezaji wote wa timu hiyo, viongozi na mashabiki ili warudi na kombe na kuwafurahisha Watanzania. Ingawa mechi hiyo itakuwa ngumu na ya ushindani wa aina yake na hasa kutokana na USM Alger kuonyesha uwezo mkubwa uwanjani na in...