PAUL NONGA KUSTAAFU SOKA MBELE YA YANGA
Wakati ligi ikitaraji kufika ukomo June 9, 2023 kwa upande wa mshambuliaji Paul Nonga wa Mbeya City amesema atahitimisha safari yake ya kusakata kabumbu katika mechi ya mzunguko wa 29 ya ligi kuu wakati timu yake ya Mbeya City FC @officialmbeyacityfc itakapoikaribisha Young Africans sports club June 6,2023.
Nje ya soka Nonga ambae jina la utani huitwa 'Baba Paroko' tofauti na kucheza mpira kitaaluma yeye ana taaluma ya kupasua miamba migodini (Blaster).
Nonga amesema amelazimika kupumzika rasmi kucheza kutokana na kuandamwa na majeraha ya muda mrefu, licha ya kupumzika bado ataendelea kuutumikia mpira wa miguu kwa upande mwingine kama kocha msaidizi wa timu yake ya Mbeya City FC kwa sasa.
Ikumbukwe Nonga ana leseni C ya ukocha ya CAF Klabu alizopita ni Yanga SC, Mwadui FC, Lipuli FC, Gwambina FC, JKT Oljoro na Mbeya City FC ambayo anaitumikia kwa mara ya pili hapo.
Pongezi kwake miaka karibia 13 ya soka sio haba kwake.