MWAKALEBELA ALIGOMEA GOLI LA PILI LA USM ALGER
Aliyekuwa makamu wa Rais wa Yanga SC, Fredrick Mwakalebela amesema bao la pili walilofungwa na USM Alger ilikuwa ni 'offside' kwa mujibu wa jicho lake la kitaalam hata hivyo wameyapokea matokeo anaamini benchi la ufundi watajipanga vyema katika mchezo wa marudiano nchini Algeria Juni 3, 2023.
“Haya ni mashindano makubwa Afrika hivyo mechi ilikuwa nzuri dakika zote tisini na Yanga imecheza vyema kuanzia kipindi cha kwanza hadi cha pili hivyo haikuwa bahati“ amesema Mwakalebela.