YANGA KUSHUSHIWA RUNGU NA CAF
Huenda klabu ya Yanga ikakutana na adhabu kutoka Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) baadaya siku ya Jana mashabiki kupata kadhia ya kuingia uwanjani Hali iliyopelekea Zaidi ya mashabiki 30 Kujeruhiwa na Kukimbizwa Hospitali Huku Shabiki mmoja Akifariki duniani.
Tukio kama hili liliwahi kuikuta Klabu ya ES TUNISIA , Baada ya vurugu za mashabiki Katika Mchezo wao dhidi ya JS Kabylie na shabiki mmoja kupoteza maisha, Es Tunis walifungiwa kucheza mechi zao bila mashabiki
Raja Casablanca nao kutoka Morocco Baada ya vurugu Kutokea kwenye mechi yao dhidi ya Al Ahly CAF Waliwafungia na kutakiwa kucheza nje ya Morocco michezo yao miwili ya mkondo wa kwanza endapo watashiriki msimu ujao.