NYOTA BARCELONA AMPATA MAMA YAKE MZAZI BAADA YA KUPOTEZANA

Mama huyu kutoka katika nchi ya Liberia aitwaye Nancy Pyne amesema Frenkie Kessie ni mtoto wake na wamepotezana baada ya mme wake kuwaomba awapeleke shule katika nchi ya Ivory Coast na baada ya hapo hawajawahi kumuona tena zaidi ya kuishia kwenye vyombo vya habari.

Mama huyo amesema waliondoka nyumbani wakiwa watoto wadogo wakiwa na kaka ake ambao wote walikuwa wadogo na baada hapo alisikia wameenda Ulaya na baba huyo alikataa mawasiliano ili wasiwasiliane tena na huku kwakua mama huyo hakuwa na uwezo wowote hakufanya kitu chochote zaidi ya miaka yote hakuwa na usingizi mzuri "Alisema hivyo"

Baba ake Frenkie na kaka ake aliwambia hawana mama ndiyo maana Frenkie Kessie alikuwa anaulizwa mama mzazi yupo wapi??? Alikaa kimya na kuwajibu kwamba hana mama, baba ndiyo aliwakuza .

Baada ya kusikia taarifa hizo Frenkie Kessie amepewa ruhusa na klabu yake ya Barcelona na ametumia usafiri wake binafsi kusafiri mpaka ufaransa kwaajiri ya kuonana na kaka yake ili kumtafuta mama huyo ili waonane nae.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA