IBRAHIM CLASS ATWAA MKANDA WA SUPER FEATHER
Ibrahim Class ameshinda Mkanda wa uzito wa kati (Super Feather) katika pambano hilo baada majaji wote watatu kumpa ushindi wa pointi 98-91, 97-92, 97-92
Akizungumza baada ya pambano hilo la Raundi 10 lililofanyika Masaki, Dar es Salaam, Class amesema “Nilijua nitampiga mpinzani wangu kwa kuwa nilishasema tangu awali kuwa huyu si Bondia bali ni mpiga debe.”
Upande wa #SaidChino amesema “Nataka nirudiane naye, Class sio mkali, ameshinda kwa kuwa kuna mambo yametokea lakini uwezo wake bado na ndio maana huwa anapewa mabondia wa mchongo kupigana nao."