YANGA YAIPORA MCHEZAJI SIMBA
Mabosi wa Klabu Bingwa Tanzania Bara Young Africans wanadaiwa kuifanyia umafia Simba SC kwa kupanda dau kwenye kuipata saini ya beki wa Ihefu FC, Yahaya Mbegu, ambaye taarifa zinasema amemalizana na Singida Big Stars.
Sasa baada ya taarifa hizo kuwepo, Young Africans wenyewe wametua huko Singida kuhamisha usajili huo kabla ya jina lake kuingizwa kwenye mfumo wa usajili wa Shirikisho la Soka Tanzania ‘TFF’.
Mbegu alijiunga na Ihefu FC msimu huu, na kujihakikishia namba katika kikosi cha kwanza, jambo ambalo timu nyingi zimeanza kumpigia hesabu.