Neymar Jr huyooo Man United
Imeripotiwa kuwa Neymar anataka kujiunga na Manchester United msimu huu wa majira ya joto na sio timu nyingine yoyote.
Ripoti kutoka Ufaransa zinadai staa huyo moyo wake wote upo Man United atakapoondoka Paris Saint-Germain na si vinginevyo.
Staa huyo mwenye umri wa miaka 31 anapitia wakati mgumu kutoka kwa mashabiki wa PSG kwa miaka kadhaa sasa ukichanganya na majeraha ya mara kwa mara hivyo anatarajiwa kuondoka dirisha hili.