ALIYEIUA YANGA KUCHEZA TIMU MOJA NA MAHREZ
Aymen Mahious wa USM Alger aliyefunga goli la kwanza dhidi ya Yanga katika fainali ya kwanza Kombe la Shirikisho Afrika ameitwa katika kikosi cha timu ya Taifa ya Algeria kitakachocheza mechi za kufuzu AFCON 2023 dhidi ya Uganda na ya kirafiki dhidi ya Tunisia.
Kwa kifupi, huyu bwana wanapasiana na Riyad Mahrez ambaye huwa anampa assist Haaland.