Makala: NI DHARAU KUBWA KUMLINGANISHA NA KAGERE

NIMETEMBELEA baadhi ya kurasa za mitandao ya kijamii hasa kwenye Facebook, Instagram na magroup ya Whatsaap ambapo baadhi ya wadau wakafikia hatua ya kuwafananisha Fiston Kalala Mayele na Meddie Kagere. 

Kilichonishangaza na kuona ni dharau kubwa waliyomfanyia mshambuliaji wa kimataifa wa DR Congo Fiston Mayele ambaye pia ni mshambuliaji tegemeo wa Yanga SC, kumfananisha Mayele na Kagere ni dharau. 

Watu walioleta ushindani huo wa Mayele na Kagere ulitokana na Kagere wa misimu minne iliyopita na Mayele wa sasa, ushindani huo wa Mayele sio na Kagere wa sasa anayeichezea Singida Big Stars kwa mheshimiwa Mwigulu Nchemba. 

Na pia simdharau Kagere, kwani ni mmoja kati ya washambuliaji hatari waliowahi kung' ara kwenye Ligi Kuu bara na kuweza kuibuka mfungaji bora misimu miwili mfululizo.

Kagere alisajiliwa na Simba msimu wa 2018/2019 akitokea Gor Mahia ya Kenya na alifanikiwa kuibuka mfungaji bora ndani ya msimu wake wa kwanza. 

Mshambuliaji huyo wa kati alivunja rekodi za Amissi Tambwe na Emmanuel Okwi ambao kila mmoja alifunga magoli 21, Kagere msimu wake wa kwanza mbali ya kuiwezesha Simba kutetea ubingwa wa bara, alifanikiwa kufunga magoli 23.

Uganda, hakuweza kufunga zaidi ya bao moja, isipokuwa Simba ilimtegemea sana Clatous Chama kwenye ufungaji na si yeye. 

Na hiyo ndio tofauti ya Kagere na Mayele, ambaye alisajiliwa na Yanga msimu uliopita akitokea timu ya AS Vita Club ya DR Congo.



Msimu wake wa kwanza Mayele alifunga mabao 16 na kushika nafasi ya pili, nyuma ya George Mpole wa Geita Gold aliyefunga magoli 17 na kuibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu bara. Ingawa alikuwa mfungaji namba mbili.

Mayele alitokea kukubalika sana na mashabiki wa soka nchini, iwe mkubwa, kijana na mtoto wote walimkubali sana Mayele.

Achana na staili yake ya ushangiliaji, Mayele ni mshambuliaji hatari kumzidi Kagere. 

Msimu huu Mayele ndie kinara wa mabao Ligi Kuu bara, kwani mpaka sasa ana mabao 16 na anayemfuatia ana mabao 10 huku ligi zikibakia mechi mbili na tayari Yanga imeshatwaa mara mbili mfululizo. 

Umahiri wa Mayele haujaishia kwenye ligi ya bara peke yake kama ilivyo kwa Kagere, Mayele amehamishia makali yake kimataifa na tayari ameisaidia Yanga kuingia fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. 

Haijaishia hapo, Mayele ni kinara wa mabao wa michuano hiyo ambapo mpaka sasa amefunga magoli 6. 

Ni dhambi kumlinganisha Mayele na Kagere. 
Asanteni





Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA