SIMBA WAMLILIA SHABIKI ALIYEFARIKI UWANJA WA MKAPA JANA

Uongozi wa klabu ya Simba umetoa salamu za pole kwa familia ya shabiki aliyefariki dunia katika msongamano wa kuingia uwanjani kwa Mkapa jijini Dar es Salaam kushuhudia fainali ya kwanza Kombe la Shirikisho Afrika baina ya Yanga dhidi ya USM Alger jana Jumapili.

“Kwa masikitiko makubwa Klabu ya Simba inatoa pole kwa familia ya shabiki aliyefariki Uwanja wa Benjamin Mkapa wakati akiwa katika jitihada za kuingia kushuhudia mechi ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika kati ya Yanga dhidi ya USM Alger ya Algeria leo (jana) Mei 28, 2023,” ilisema taarifa hiyo.

Shabiki huyo alikuwa miongoni mwa watu 30 waliojeruhiwa na kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Temeke ambapo alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI