MOHAMED KACHUMARI AFARIKI DUNIA
Beki wa zamani wa timu ya Kikwajuni, Small Simba, Mlandege na Mafunzo, Moh'd Kachumbari amefariki Dunia asubuhi ya leo Jijini Dar es Salam.
Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa mchana huu kutoka Dar kwenda kuzikwa nyumbani kwao Zanzibar.
Marehemu Kachumbari pia aliwahi kucheza timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) na Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars).
Inallillah Wainailah Rajiun, Mwenyezi Mungu amsamehe makosa yake 🤲.