YANGA KUKABIDHIWA UBINGWA WAO SUMBAWANGA JUNI 9
Bodi ya ligi kupitia kwa afisa hahari wake, Karim Boimanda imesema kuwa, Klabu ya Yanga watakabidhiwa Ubingwa wao wa ligi kuu Juni (9) Mjini Sumbawanga.
» Watakabidhiwa kwenye Mchezo wa ligi kuu dhidi ya klabu ya Tanzania Prisons ambao wamechagua kamalizia mechi zao katika dimba la Nelson Mandela Sumbawanga.
» Pia bodi imeeleza kusikia ushauri wa baadhi ya wadau wa soka kuhusu ratiba ngumu inayoikabiri klabu ya Yanga. Bodi hiyo imesema muda ni mfinyu ligi inatakiwa kumalizika Juni (9) hivyo ratiba itabaki vilevile, hakuta kuwa na mabadiliko.
» Mchezo wa fainali ya (FA) baina ya Azam dhidi ya Yanga utachezwa tarehe ileile Juni (12) katika uwanja wa Mkwakwani Tanga.