ZITTO KABWE KUMALIZA TOFAUTI ZA ALI KIBA, DIAMOND PLUTINUMZ
Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, amejitosa kusuluhisha ugomvi wa muda mrefu wa wasanii wawili wa muziki wa kizazi kipya nchini, Ali Kiba na Nasibu Abdul 'Diamond'. Zitto alitoa kauli hiyo juzi wakati akihojiwa katika Kipindi cha Mkasi kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha EATV baada ya kuulizwa kuwa ni jitihada gani amezifanya kusuluhisha ugomvi wa wasanii hao akiwa kama mlezi wa wasanii wanaotoka mkoani Kigoma.