Ruka hadi kwenye maudhui makuu

KROOS, RODRIGUEZ KUANZA DHIDI YA SEVILLA

Toni Kroos

Kocha wa Real Madrid, Carlo Ancelotti, amedhibitisha ataachilia mizinga yake mizito ikiwemo nyota wapya Toni Kroos na James Rodriguez kwenye kombe la Uefa Super dhidi ya Sevilla Jumanne.

Viungo hao wa kati walianza mazoezi Agostu 5 baada ya kuibuka mashujaa katika Kombe la Dunia, Rodriguez kwa Colombia na Kroos kwa mabingwa wa dunia, Ujerumani lakini Ancelotti alisema wote wataanza kivumbi hicho kitakacho toa vumbi jijini Cardiff.

“Ndio, wote watakuwa kwenye orodha ya watakaoanza,” alijibu alipoulizwa ikiwa atawatumia nyota hao.
Kroos anatarajiwa kushirikiana na Luka Modric kati kati mwa kiwanja huku Rodriguez akicheza nambari 10.

Ancelloti alitangaza kwamba nyota wa Ureno, Cristiano Ronaldo, atashiriki kutoka kipenga cha mwanzo licha ya kusumbuka na jeraha sugu la goti katika Kombe la Dunia.


“Hana tatizo lolote, alishiriki mazoezi ya kiwango cha juu kabisa na wenzake na naamini kuwa ako katika hali nzuri,” mwalimu huyo aliambia kongamano la wanahabari jijini Cardiff.

Nyota maarufu wa Wales, taifa ambalo mechi hiyo itaandaliwa, Gareth Bale ambaye ni mechzaji ghali zaidi duniani anatarajiwa kuanza kwenye kikosi hicho ndoto ya wengi lakini Ancelotti akifanyia wanahabari wa nchi hiyo mzaha kuhusu mwana wao mashuhuri zaidi duniani.

“Sijui kama atacheza kwani kila mmoja hapa anasema, amerudi nyumbani! Amerudi nyumbani!” kocha huyo alinena.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limetoa orodha ya viwango vya ubora wa klabu barani, Simba ikiendelea kuwa juu ya klabu nyingine za Tanzania, nafasi ya tano. Orodha hiyo imetoka leo kuelekea droo ya hatua za awali za michuano ya klabu Afrika ambayo kwa mara ya kwanza kihistoria itafanyika nchini katika studio za Azam Tv, Tabata Jijini Dar es Salaam. Yanga ambayo kama Simba itashiriki Ligi ya Mabingwa — yenyewe inashika nafasi ya 12, wakati timu nyingine katika orodha hiyo ni Namungo FC wanaoshika nafasi ya mwisho, ya 75 kwa pamoja na Salitas FC ya Burkina Faso, Ahli Benghazi ya Libya na NAPSA Stars ya Zambia. Kwa msimu ujao mbali na Simba na Yanga kushiriki Ligi ya Mabingwa, Azam FC na Singida Black Stars zitashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

Miongoni mwa viungo wa pembeni wanaofanya vizuri ni Benodict Khalfan Ngassa ambaye amekuwa akifanya vizuri. Ngassa ambaye ni mtoto wa mchezaji wa zamani wa Pamba Jiji na Simba SC, Khalfan Ngassa, pia ni mdogo wa kiungo mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Simba na Azam, Mrisho Ngassa anatajwa ni mmoja kati ya wachezaji wanaotazamiwa kufanya makubwa siku za usoni. Mambo Uwanjani Blog itawaletea Makala maalum ya kiungo huyo hatari ambaye ndoto zake ni kufuata nyayo za kaka yake Mrisho Ngassa. Beno Ngassa