DROGBA ARUDI NA MGUU MBAYA CHELSEA, ASHINDWA KUNG'ARA
Mshambuliaji
huyo wa Ivory Coast, aliichezea kwa mara ya mwisho Chelsea mwaka 2012
katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, ikishinda kwa penalti dhidi ya
Bayern Munich, lakini leo akirejea Ujerumani yeye na washambuliaji
wengine wa The Blues- walilala kwa mabao ya Ludovic Obraniak kwa kichwa
na penalti za Assani Lukimya na Felix Kroos.
Kipa wa Chelsea, Thibaut Courtois amefungwa mabao mawili leo, wakati bao lingine alifungwa Petr Cech kipindi cha pili