Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho
Chelsea ilipeleka kilio kwa
Burnley usiku wa jumatatu katika mchuano wa ligi kuu ya England ambapo
Chelsea iliitandika Burnley mabao 3-1.
Burnley ilitangulia kufunga bao moja dhidi ya
Chelsea kupitia mchezaji wake Scott Arfield katika kipindi cha kwanza
cha mchezo hali iliyotishia kuwa pengine Chelsea ingepoteza katika
mchezo huo, hata hivyo , goli hilo halikudumu kwa muda mrefu,ambapo kazi
nzuri ya wachezaji wa Chelsea kama vile Diego Costa,Ivanovich na Andre
Shule ilitosha kabisa kuitoa jasho Barnley.