DI MARIA RASMI MANCHESTER UNITED

Manchester United wamemsajili winga wa Real Madrid Angel Di Maria kwa kitita cha pauni milioni 59.7, ambayo ni rekodi ya uhamisho Uingereza.

Winga huyo kutoka Argentina, amefanya vipimo vya afya siku ya Jumanne asubuhi na kusaini mkataba wa miaka mitano.
Di Maria huenda akacheza mechi yake ya kwanza siku ya Jumamosi dhidi ya Burnley katika mchezo wa Ligi Kuu ya England.

Ada hiyo ya uhamisho inazidi ada ya pauni milioni 50 iliyotolewa na Chelsea kumsajili Fernando Torres kutoka Liverpool mwaka 2011.

Di Maria aliishuhudia timu yake mpya ikizabwa mabao 4-0 na kitimu cha daraja la nne katika michuano ya Capital One hivyo Mna United imetupwa nje kabisa, ujio wa nyota huyo kunaweza kuifanya ibadili matokeo na kuanza kufufua matumaini yake mapya baada ya kuendelea kusuasua, Man United imeanza ligi ya premia ambapo imepoteza mechi moja na kutoka sare mojana ina pointi moja tu.


Di Maria huenda akacheza dhidi ya Burnley mechi inayofuata sasa dhidi ya mshetani hao wekundu waliopoteza mvuti mbele yamashabiki wao

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA