NISHA, MBOTO WAJIWEKA JUU NA FILAMU YAO YA KIDUME

Mastaa wa filamu nchini Salma Jabu Nisha na Mboto wamekuja na filamu mpya inayoitwa Kidume ambayo tayari ipo sokoni tangu juzi. Nae Nisha ameandika"Si muda mrefu tangu ZENA NA BETINA itoke,..ila linapokuja swala la jamii yangu huwa nasitisha lolote ili niweze kujitoa, pengine hutojitoa kwa pesa,ila unaweza kufanya kitu ukatengeneza pesa kwa ajili ya kusaidia kitu hiko, wenye imani (wakristo safi/Islam safi) huwa tunaamini ukitoa mkono wa kulia wa kushoto usione, nilijifunza hilo mwanzoni mwa mwaka huu moja ya comment ya shabiki yng humu
humu instagram,.

Kwa kuwa huwa napenda sana kusikiliza ushauri bora basi na huo ni kati ya shauri bora nililolifanyia kazi,nirudi kwenye mada ‪#‎KIDUME‬ "KIDUME" ni filamu ambayo imenifanya niandike yote haya sababu tulijitoa kwa ajili kufanya watu fulani wanaolia wapate afueni, wenye mateso ya muda mrefu


kama hatutaweza kuwaponyesha sababu uponyaji ni wa M'Mungu tu na msaada wa daktari, basi pesa itakayopatikana ktk filamu hii iweze kusaidia kwa kiasi fulani (mkono wa kushoto usione,na pia saa nyngn unafunza wengine sababu we ni kioo wajitazame kwa vilivyo bora).

chanzo swahiliworldplanet

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA