WENGER ASHANGAZWA NA MTANDAO WA KLABU YA MAN CITY



Meneja wa Arsenal Arsene Wenger Jumapili alieleza kushangazwa kwake na mpangilio ambao umewezesha kiungo wa kati wa zamani wa Chelsea Frank Lampard kujiunga na klabu ya Manchester City kwa mkopo kutoka kwa ‘klabu-dada’ ya New York City.

Pamoja na kuhamia kwa Lampard uwanja wa Etihad, New York pia wamemkopesha straika wa Uhispania David Villa kwa Melbourne City.

Klabu zote tatu zinamilikiwa na City Football Group, kampuni inayomilikiwa na wamiliki wa City, Abu Dhabi United Group.

Wenger, ambaye timu yake itakabiliana na City wikendi ijayo kupigania Community Shield, alidokeza kwamba ushirika huo huenda ukawapa mabingwa hao wa Ligi ya Premia nafuu wasiyofaa.


Alipoulizwa kuhusu kuhama kwa Lampard, alijibu: “Inanishangaza. Ni kama hizi klabu za ‘City’ zitalisha klabu kuu, Man City. Nilisikia wanataka kununua klabu tano kote duniani.

“Ninafahamu sheria vyema. Walinunua klabu (New York City) kwa $100 milioni (euro 74 milioni) Marekani ya kucheza msimu ujao.

"Kwa sasa, wachezaji wanaowanunua hawawezi wakacheza hadi mwaka ujao, kwa hivyo wanawasajili katika klabu hizo na wanaweza kuwatoa nje kwa mkopo.

“Ni njia ya kukwepa sheria (za shirikisho linalosimamia soka Ulaya Uefa) za uchezaji haki kifedha? Sijui.”

Alipouliza kama Arsenal ingependa kuanzisha mtandao wake kama huo wa klabu, alijibu: “Tunafurahia kutumia pesa tunazotengeneza kuendesha klabu yetu. Hatuna pesa nyingi za ziada za kununua klabu nyingine.”

Wenger alikuwa akihutubu katika kikao cha wanahabari baada ya timu yake kushindwa 1-0 na Monaco katika dimba la kirafiki la Kombe la Emirates katika uwanja wa Emirates wao Arsenal.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA