LIVERPOOL YAICHAKAZA DORTMUND 4-0, COUTINHO ANG'ARA
Mshambulizi wa Liverpool Dejan
Lovren aliifungia the Reds bao lake la kwanza katika mechi yake ya
kwanza Liverpool ilipoilaza Borussia Dortmund mabao 4-0 katika mechi
ya kirafiki.
Daniel Sturridge ndiye aliyeifungua kivuno hicho cha mabao baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Phillippe Coutinho.Lovren, aliyejiunga na ''the Reds'' akitokea Southampton, katika kandarasi ya pauni milioni 20m alifuma bao la pili kwa kichwa alipotumia vyema kona kutoka kwa Steven Gerrard .
Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers aliwachezesha wachezaji wapya Lovren, Javier Manquillo, Emre Can Rickie Lambert katika mechi hiyo.
Liverpool, itafungua kampeini ya msimu huu dhidi ya Southampton jumapili ijayo.
Dortmund itafungua kampeini yake dhidi ya Bayer Leverkusen tarehe 23 Agosti.