PHIRI AAHIDI UBINGWA MSIMBAZI, MAXIMO AMTUNISHIA MISULI
Wakati Kocha Mkuu wa Simba, Mzambia Patrick Phiri akidai ubingwa bila kuifunga Yanga hauna raha, Marcio Maximo ametamba kutumia kikosi mseto cha wakongwe na chipukizi kwenye Ligi Kuu Bara iliyopangwa kuanza Septemba 20, mwaka huu.
Akizungumza na gazeti hili kabla ya kuondoka kuelekea visiwani Zanzibar mwishoni mwa wiki ambako Simba imeweka kambi ya kujiandaa na msimu mpya, Phiri alisema moja ya mikakati aliyojiwekea ni kuhakikisha anatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara lakini hautanoga bila kuifunga Yanga.
"Moja ya mikakati niliyojiwekea ni kuhakikisha Simba inatwaa ubingwa wa ligi ikiwa chini yangu, lakini nitafurahi zaidi nikitwaa ubingwa na kuifunga Yanga," alisema Phiri.
Alisema msimu huu amejipanga kuhakikisha anairejesha raha iliyopotea kwa muda mrefu Msimbazi kwa kuwa mikakati yake ya kwanza ni klabu hiyo kufanya vizuri katika mechi za mzunguko wa wa kwanza na badaye kuhitimisha kwa kutwaa ubingwa.
Phiri ambaye awali katika msimu wa 2004/05 aliipa Simba ubingwa kabla ya ule wa 2009/10 kuhitimisha kwa kutwaa ubingwa bila kupoteza mechi, alisema amejipanga kutoa mazoezi ya makini katika idara zote ili kuwaweka sawa wachezaji wake kabla ya kuanza kwa ligi hiyo.
Mzambia huyo aliondoka jijini Dar es Salaam jana kuelekea Zanzibar kuungana na kikosi cha timu hiyo kwa ajili ya kuendelea na mazoezi ya kujiandaa na Ligi Kuu ya Bara.
Wakati Phiri akieleza hayo, Maximo alisema kikosi chake kipo kamili na mazoezi ya kujiandaa na Ligi Kuu ya Bara na kwamba mazoezi ambayo wameshafanya yamekamilika na kilichobaki ni kurekebisha kasoro ndogo ndogo.
"Timu ipo kamili kwa sasa, imebaki kiasi kidogo kukamilisha mazoezi tayari kwa kuanza Ligi Kuu," alisema Maximo.
Alisema amejipanga kuhakikisha Yanga inafanya vizuri katika michuano hiyo na kutwaa ubingwa ambao kwa sasa unashikiliwa na Azam FC ya jijini Dar es Salaam.
Simba na Yanga zote zimeweka kambi visiwani Zanzibar kwa ajili ya kujiandaa na Ligi Kuu Bara huku mabingwa watetezi Azam FC wakiitumia michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame) kujiwinda na Ligi Kuu.