MIMI SIYO FREEMASON- HOZA

MTENDAJI mkuu wa mtandao wa Mambo Uwanjani blogspot, Prince Hoza amekanusha vikali kuwa yeye si muumini wa dini ya kishetani ya Freemason tofauti inavyoelezwa kuwa anashiriki kuunganisha watu katika imani hiyo.

Hoza amedai watu wengi wamekua wakimpigia simu ili awaunganishe katika imani hiyo inayodaiwa ni ya kishetani na inayowapa watu utajiri, akizungumza na Mtandao huu, Hoza amesema yeye si freemason isipokuwa ameshiriki kuandika habari za freemason hivyo asihusishwe  kabisa na imani hiyo.

'Unajua watu si waelewa, niliandika habari moja ambayo nilifanya mahojiano na msanii mmoja ambaye anadai yeye ni memba wa freemason, hivyo niliitoa katika mtandao huu na kuweka jina langu kama mwandishi, nashangaa baada ya hapo watu wengi wamekuwa wakinipigia simu wakitaka niwaunganishe', alisema na kuongeza.


'Sipo kabisa katika imani hiyo kwanza sijui iko wapi', anasema Hoza, aidha amewataka wasomaji kutambua kuwa yeye ni mwandishi tu na wala si muumini wa dini hiyo, Hoza alifanya mahojiano na msanii wa muziki wa kizazi kipya Mkola Man ambaye alijitambulisha kuwa ni memba wa freemason.

Hivyo mmeombwa kutomwelewa vibaya Hoza ambaye ameanza kuwatia mashaka baadhi ya watu wake wa karibu ambao wanaamini na yeye ni mfuasi wa imani hiyo ya kishetani ambayo inadaiwa kuhusisha ushirikina.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA