MANENO YA DIAMOND YAMLIZA AUNT EZEKIEL

Star wa filamu nchini Aunty Ezekiel anadaiwa kuchomwa vilivyo na maneno ya Diamond kwa Wema Sepetu yanayodaiwa kumgusa yeye pia moja kwa moja kama rafiki wa Wema, Diamond juzi alisema  kuwa Wema anapenda sana starehe na mashoga wapenda kujirusha badala ya kufanya kazi ili kujiletea maendeleo kwa kutumia fursa aliyonayo sasa.

Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na Aunty kikizungumza  jana kwa masharti ya kutotajwa jina kilisema kuwa baada ya Aunty kuona alichoandika Diamond aliachia msonyo wa kufa mtu kuonyesha hakupendezwa hata kidogo huku akibaki kuumia.

"Aunty alipoona alichoandika Diamond alichia msonyo huo ! unajua maneno ya Diamond yamejaa ukweli mtupu, yalikuwa kama mkuki kwa Aunty, Aunty ni mtu wa starehe sana si umeona hata ndoa yake haina uhai, ukweli unauma, yeye na Wema wanapaswa kujiangalia upya Diamond amempa Wema ushauri mzuri sababu anampenda"


Chanzo hicho kilisema kuwa Aunty anataka kukata ukaribu wake na Wema ili kuepusha maneno kwasababu ameshazoea kuishi kwa kujirusha

"Urafiki wa Wema  na Aunty muda si mrefu utakuwa kama ule wa Kajala, Aunty anataka kumuacha Wema na bwana'ke yeye achukue hamsini zake" kilisenma chanzo hicho

Hata hivyo Aunty alipotafutwa ili kutoa ufafanuzi hakupatikana kwa wakati.

Chanzo Swahiliworldplanet

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA