RUDISHA AAMBULIA MEDALI YA FEDHA GLASGOW
Bingwa wa Olimpiki na ambaye pia
anashikilia rekodi ya dunia katika mbio za mita 800 mkenya David
Rudisha aliambulia medali ya fedhakatika mashindano ya Jumuiya ya
madola.
Amos, ambaye alishinda medali ya fedha katika mashindano ya olimpiki mjini London alimaliza mbio hizo kwa kishindo baada ya kutoka nyuma ya Rudisha na kumpiku.
Kwa kawaida, Rudisha alikuwa mbele wakati wa mbio hizo kwa mita 150 na kudhibiti mbio zenyewe kama alivyofanya alipovunja rekodi mwaka 2012.
Lakini alikiri kuwa mbio hizo hazikuwa ngumu , ila mita miamoja za mwisho ndizo zilizomtatiza na hapo ndipo Amos aliweza kumpiku Rudisha.
Alionekana kuishiwa na nguvu wakati Amos kutoka Botswana alipompiku na kuanza kusherehekea na kushinda dhahabu.
Rudisha mwenye umri wa miaka 25 alimaliza mbio hizo kwa dakika 1:45.48 nyuma ya Amos huku Andre Olivier wa Afrika Kusini akinyakua Shaba.
Amos aliambia BBC kuwa ana raha sana ingawa Rudisha daima atasalia kuwa bingwa wa mbio za miata 800.
Mbio hizo zilikuwa moja ya mbio zilizosubiriwa kwa hamu kuu katika mashindano hayo ya Jumuiya ya madola.