MARADONA AMPIGA MAKOFI MWANAHABARI

Diego Maradona

Mstaafu wa soka nchini Argentina, Diego Maradona, amenaswa kwa kanda ya picha akichapa mwanahabari Jumamosi kulingana na runinga ya Sky Sports.

Makabiliano hayo walitokea wakati gwiji huyo, 53, alikuwa akiondoka kutoka ukumbi wa maonyesho ya sanaa na mwanaye ambaye alikuwa ameenda kutizama tamthilia ya Siku ya Watoto ya Argentina.

Imeripotiwa kuwa mwanahabari mhusika alikunjia jicho mamake mwana huyo ambaye ni mpezi wa kitambo wa Maradona, Veronica Ojeda.

Maradona, ambaye alishinda Kombe la Dunia kama mchezaji 1986 na kuongoza taifa lake kama kocha kutoka 2008 hadi 2010, ana uzoefu wa kuzozana na wanahabari.


Alipewa kifungo cha gerezani cha nje kwa miaka miwili na miezi 10 mwakani 1994 kwa kufyatulia wanahabari bunduki ya hewani nje ya nyumba yake ambapo watu wanne walijeruhiwa.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA