CHELSEA KUMENYANA NA BURNLEY
Ligi kuu ya England ambayo
imeanza jumamosi iliyopita itaendelea jumatatu hii ambapo Burnley
watawakaribisha Chelsea kwenye uwanja wa Turf Moor.
Chelsea wao huenda kocha Jose Mourinho akawaanzisha wachezaji wake wapya Cesc Fabregas, Diego Costa na Filipe Luis na bila shaka golikipa Thibaut Courtois.
The Blues wana nafasi ya kujaribu uimara wa goti la mkongwe Didier Drogba, huku wachezaji wengine kadhaa wakielezwa kuwa na hofu ya majeraha.