JESHI KAMILI LA NOOIJ TAYARI KUIVAA MOROCCO

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mholanzi Mart Nooij ametangaza kikosi cha wachezaji 26 kwa ajili ya mechi ya kirafiki dhidi ya Morocco iliyopangwa kufanyika Septemba 5, mwaka huu nchini humo.

Wachezaji walioitwa kwa ajili ya mechi hiyo ambayo ipo katika Kalenda ya Fifa ni makipa Deogratius Munishi (Yanga) na Mwadini Ali (Azam). Mabeki ni Said Morad (Azam), Oscar Joshua (Yanga), Shomari Kapombe (Azam), Nadir Haroub 'Cannavaro' (Yanga), Kelvin Yondani (Yanga), Aggrey Morris (Azam), Joram Mgeveke (Simba) na Charles Edward (Yanga).

Viungo ni Erasto Nyoni (Azam), Mwinyi Kazimoto (Al Markhiya, Qatar), Amri Kiemba (Simba), Himid Mao (Azam), Salum Abubakar (Azam), Said Ndemla (Simba), Said Juma (Yanga) na Haruna Chanongo (Simba).

Washambuliaji ni John Bocco (Azam), Khamis Mcha (Azam), Simon Msuva (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC), Mrisho Ngassa (Yanga), Mwegane Yeya (Mbeya City) na Juma Liuzio (Zesco, Zambia).

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirikisho la soka nchini (TFF), wachezaji hao walioitwa wataingia kambini Jumapili wiki hii kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo wa ugenini dhidi ya timu ya Taifa ya Morocco.

Morocco katika mechi hiyo itakuwa sehemu ya maandalizi ya fainali za Afcon mwakani ambayo itakuwa nchi mwenyeji.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA